1. Intro :: Jifunze ketengeneza Blog na weka Biashara yako Online

Karibu,

Kutengeneza Blog sio kazi ngumi kama watu wanavyofikia, ni rahisi sana unachotakiwa kujua ni taaluma ndogo tu computer na jinsi ya kutumia Internet.


Ukiwa na Blog yakwako unaweza ukafanya mambo mengi tu kama vile :

1. Kutangaza Biashara yako au ya mtu mwengine.
2. Kutunza taarifa zako kwenye mtandao na ukaamua nani azione na nini asizione.
3. Kutengeneza online community uitakayo kutokana na malengo yako.
4. Kutoa taarifa kwa ulimwengu juu ya jambo fulani.
5. Kujibrand na kazi yako mfano mzuri kama millardayo kwenye millardayo.com.

Na mengine mengi unaweza ukayakamilisha kupitia Blog.

Tatizo ni kwamba watu wengi wanataka kufanikiwa kwenye hili, lakini hawajui wapi waanzie, Ila hapa tutakuelekeza jinsi ya kufanya mpaka ukawa na blog yako yenye muonekano mzuri uutakao.

Blog ina vitu vingi sana ila tutajitahidi kukava vile vitu muhimu vitakavyokusaidia kutengeneza Blog yenye muonekano mzuri.

Kitu cha kwanza muhimu kwenye Blog ni kuchagua jina la Blog yako, jina lina mchango mkubwa katika kuifanya Blog yako ipendwe na watu. Unapochagua jina hakikisha unachagua jina linawezwa kusomwa kiurahisi na watu, Kila siku watu wapya wanatengeneza Blog na wanachagua majina wayatakayo hivyo kuna uwezekano ukachagua jina ambalo lishapata mtu tayari kwenye hali kama hiyo itakubidi uchague jina lingine. Mfano unataka Blog yako iitwe matukio.blogspot.com unaweza ukaambiwa hii blog ina mtu tayari ikimaanisha huwezi kutumia hilo jina kwenye Blog yako, Chakufanya hapo ni kutafuta jina jengine au kuongeza herufi au namba kwenye jina hilohilo mfano baada ya matukio.blogspot.com ukaweka matukioTz.blogspot.com.


Pili, ni kuchagua template au sura ya Blog yako, sura ya blog ni muhimu sana kwasababu watumiaji siku zote watapenda kitu kizuri chenye kuvutia. Template ziko nyingi online na nyengine zinauzwa na zipo nyingi za bure cha kufanya ni kuchagua unayoitaka na kuanza kuicustomize (kuiweka kwenye muundo au mtindo unaoutaka).


Tatu, ni jinsi ya kutengeneza menu yako kwenye Blog, menu ni mtingo wa links zako zitakavojipanga kwenye Blog. Unaweza ukatengeneza menu kwakutumia label au pages, tutafahamishana hivi vyote.


Nne, tutafundishana jinsi ya kuunganisha Blog yako na Instagram, Facebook na mitandao mengine.
Ukiunganisha Blog yako na mitandao ya kijamii (social netwoks) utapata nafasi kubwa ya kuifanya Blog yako iwe maarufu haraka kwa sababu watu wako wa facebook na instagram wanaweza kulike makala, picha na vitu vyako vingine viliopo kwenye Blog.


Pia kuna vitu vengine vingi tutakava mbeleni. 

Usione tabu kuuliza endapo kuna sehemu hujaelewa, unaweza ukauliza kupitia comments au kwenye facebook page ya chekananenepa au Instagram Direct @chekananenepa.

0 comments: