Nenda kwenye address ya blogger.com na ingia (signin) kwa akauti yako kama huna tengeneza akaunti.
Baada ya Signin, Bonyeza New Blog button.
Andika title ya Blog yako na address, na chagua template uitakayo (muoneka wa blog yako).Title ni lile neno litakalooneka pale Blog yako ikifunguliwa na address ni link au url ambayo watu wataitumia kufika kwenye Blog yako.
Hapo itaona Blog tayari imeshatengezwa ila haina post yeyote. Pia unaweza ukabonyesha view blog kuona muonekano wa blog yako kutokana na template uliyochagua.
Bonyeza title ya Blog yako kuingia kwenye Blog
Kwenye menu kushoto utakuta links tofauti ambazo zinaweza kukusaidia kwenye kuboresha blog yako. Unaweza ukaenda kwenye setting na kubadili title ya blog au address, Unaweza ukaenda kwenye template kubadili muonekano wa Blog yako, Layout inatumika kupangilia matabaka la Blog na mtindo wake.
0 comments: